
Mbunifu Bi KHADIJA Mwanamboka akiwa na mmoja wa watoto wanaolelewa na chama hiko.
Hivi unafahamu Chama kisicho cha kiserikali TANZANIA MITINDO HOUSE (TMH) kilipoanzia Unaemuona pichani hapo chini ni aliekuwa Katibu muanzilishi kipindi dESIGNER HAJI MOHAMED ama wengi wanamfahamu kama HAJIBOSTON.

Yeye na Khadija Mwanamboka kwa pamoja walisimamia kwa kila hali kuhakikisha chama kinasajiliwa.
Walifanikiwa kusajili na chama kiliaanza shughuli zake baada ya kukamilika kwa usajili wake.
Show ya kwanza walioifanya ni ile ilioitwa WATOTO EXTRAVAGANZA SHOW ambao iliwashikilisha madesigner kadhaa akiwamo Fatma Amour,Masoud ali wa kipanya,haji mohamed na Khadija mwanamboka lengo kubwa ilikuwa ni kutunisha mfuko kwa ajili ya kuchangiwa watoto yatima.
Wiki moja baada ya show Katibu alikwenda masomoni nchini marekani kwa ajili ya kuongeza elimu ya art mpaka hivi bado yuko masomoni.
Kwa sasa TANZANIA MITINDO HOUSE imepiga hatua kidogo na kupata misaada mbalimbali
Mwenyekiti wa TANZANIA MITINDO HOUSE Bi Khadija Mwanamboka inamtakia kila la kheri katibu wake wa zamani huko masomo ili arudi nyumbani salama kuja kuendeleza kile walichokianza .

aliekuwa katibu kipindi hiko akisoma risala fupi kwa wageni waalikwa kwa niaba ya mwenyekiti wake Bi khadija Mwanamboka.
siku ya ufunguzi wa kwanza chama hiko ambako ulifuatiwa na FASHION SHOW YA WATOTO.
No comments:
Post a Comment