...

...

Tuesday, September 8, 2009

MADOKTA WENGINE BWANA..‏





Kuna Dr. mmoja alinichekesha sana siku hiyo, ni mwalimu wangu wa Microbiology (elimu ya viumbe vidogodogo kama bakteria, virusi, na protozoa). Wiki moja kabla ya mtihani wake wa nusu muhula alitupatia maswali ya kujipima kama 140 hivi. Nikawachkusanya waaminifu wangu na kuyafanyia kazi, baada ya siku mbili tulikuwa na majibu sahihi yote. Tulipoingia kwenye chumba cha mtihani tulipewa maswali 50 ya kuchagua (multiplechoice), hakuna kujadili, kuelezea wala kuchora. Na mbaya zaidi maswali yote 50 yalikuwa yanatoka katika yale maswali 140 ya kujipima. Nilishangaa na kujiuliza kama naota au vipi, nikajikunja na mtihani.







Leo anarudisha majibu anasema "nashangaa kumbe darasa langu kuna majiniazzz. watu watatu wamepata 100%..." Mwanaume nikawa nacheka kwa jino la kushoto tu huku nimepoa baridiii. Mi nikajiuliza alikuwa anatarajia nini pale aliporudia maswali yaleyale aliyotupatia wiki moja kabla. Mi nilijua darasa zima litakuwa na 100%. Tatizo lake hajui kuwa darasani kuna Mbongo aliyezoea kusoma kwa shida kule uswahilini, alisoma kwa mishumaa, taa za karabai na juu ya tofali badala ya dawati. Hajui kuwa mwaka ' 98 Mbongo huyu alishiriki ku-kremu majibu ya mitihani ya taifa kidato cha nne na kupelekea baraza la mitihani kufuta matokeo baada ya kugundua kuwa imevuja kupita kiasi. Na wala hajui kuwa Mbongo anaweza kutunga wimbo ili kukariri majibu au fomula fulani. Jamani ehh kuna kichwa hicho kimetoka India si mchezo. Yaani hasomi kwa ajili yake bali anasomea kijiji kama si nchi yake. Anasoma sana huyu baba na yuko fiti kichwani si kawaida. Yuko mwingine kutoka Japan, ni mzembe mzembe kwa kila jambo ila ukimpeleka darasani utakoma kuringa. Hawa wawili wananinyima usingizi...!!!!!
Kuna m-Kenya mmoja ingawa nae mwenzangu na mimi tunajikongoja, na Mmarekani huyu akiamua kusoma yuko fiti ila kinachomponza ni starehe nying, hana muda wa kushika kitabu mpaka siku mbili kabla ya pepa.

Here I remain kama maji ya Mtungi
hmtu.(houston)

No comments:

Post a Comment