...

...

Sunday, November 8, 2009

Nature, Afande kuchangia wahanga milipuko Mbagala



Nyota wa muziki wa kizazi kipya Juma Nature na Afande Sele wanatarajia kurekodi wimbo wa kulilia waliopatwa na maafa yaliyotokana na milipuko ya mabomu kwenye kambi ya jeshi iliyopo Mbagala, Dar es salaam na wamewataka wasanii kufanya onyesho la hisani kuchangia waathirika hao.

Rapa wa Morogoro Afande Sele amesema kwa njia ya simu jana kuwa alikutana na Nature juzi Ijumaa wakati wakitumbuiza kwenye sherehe ya kukabidhiwa mabasi kwa timu za Simba na Yanga na wakajadili juu ya uzito wa athari za milipuko hiyo.


``Nature ameniambia kuwa naye ni mmoja wa waathirika wa milipuko ile.

Ni jambo kubwa sana, watu wengine wanachukulia wepesi, lakini ni tatizo kubwa sana.

Watu wamepoteza maisha, wengine wameachwa na ulemavu wa maisha, wengine wameachwa wakiwa masikini kabisa hawana hata pa kulala, na viongozi wa nchi wasilichukulie poa suala hili ni zito kuliko wanavyofikiria.

``Kuna matukio mengi yanasababishwa na uzembe na yanawaathiri wananchi, hivi ni vitu vya kuchukuliwa hatua. Kwanini kambi kama ile isiende kuwekwa huko maporini? Kuna mapori mangapi hapa nchini?`` alisema.

No comments:

Post a Comment