...

...

Tuesday, September 1, 2009

MBWA NI BORA..!!?



Nimekuja kugundua kuwa thamani na hadhi ya mbwa ni bora zaidi ya binadamu mwanaume.! Hii ni jamii ya Marekani ambayo inathamini wanyama wake zaidi ya watu wake hasa wanaume, katika kila jamii duniani kuna vyeo, ubora na thamani fulani hivi wanayopewa wanajumuia husika. Hata sheria za jamii zinaegemea zaidi juu ya ubora na hadhi ya kiumbe hicho, sasa ukifuatilia jamii ya hawa ndugu zangu utaona kuwa thamani ya maisha kwa viumbe iko kama ifuatavyo..

1. Namba moja ni mtoto. Watoto wanathaminiwa kuliko kiumbe yeyote ndani ya Marekani, kila mtu anajaribu kuwalinda na sheria ndio usiseme. Hawapigwi makonzi, hawafinywi, hawasemwi wala kutolewa ukali. Mtoto wako mwenyewe ukimsema tu anapiga simu polisi na kukulundika lupango, eti wanaita Child abuse.

2. Namba mbili ni mwanamke. Thamani ya mwanake ni ya pili huku tuliko, hawa watu wana sauti, mamlaka na heshima ya kila aina. kama malkia fulani hivi. Usiombe ukagombana na mwanake ujue jamii nzima itakutenga. Na mahakamani ndio wanapeta kabisaaa, wao wanaita Sex abuse.

3. Namba tatu inashikiliwa na wanyama, wanaita pets. Hapa utawakuta kina waheshimiwa mbwa, Mr. paka, bwana mkubwa kasuku na kila aina ya mnyama. Wanyama hawa wanaheshimiwa zaidi ya tunavyomuheshimu baba mwenye nyumba kule kwetu Bongo. Mi naogopa sasa. Unaweza kuingia kwa mtu ukakuta baba kakaa chini na paka amelala juu ya kochi miguu juu! Nilipokuwa dogo, paka na mbwa wasikatize upeo wa macho yangu lazima niseme nao kwa mawe, huku mbwa ni bwana mkubwa.

4. Nafasi ya nne inashikiliwa na mwanaume.! loh hii haijakaa vizuri na siikubali. Thamani ya mwanaume ni ndogo sana kulinganisha na mnyama? Yaani mwanaume hana hadhi katika jamii hii na sheria zinamkandamiza.

Iwe ni msaada, kipaumbele au chochote kwanza anafikiriwa mtoto, halafu mwanamke, baadae mnyama (mbwa na paka) na mwisho ndio mwanaume. Na urijali wetu, na kila sifa zetu hazina nafasi katika jamii hii. Haya kina baba mpooooo??

No comments:

Post a Comment