wakati Rais wa Zanzibar Dk. Ali Mohamed Shein akiapishwa uwanja wa Amaan

Obamaz mtoto, asalaam aliekhum....
Kwa heshima na taadhima nipeperushie swala langu hili. Pia naomba unitafutie picha muafaka ziende na huu waraka wangu. Unajua, kumekuwepo na mawazo na hisia mbalimbali juu ya mustakabali wa ndugu zetu wa Kizanzibari ambao baada ya uchaguzi mkuu uliojaa vurugu wa mwaka 2000 wengi walitorokea nje ya nchi kunusuru maisha yao kwa kile kilichoonekana kukosekana kwa usalama wa maisha yao.
Wiki hii tumeshuhudia historia ikiandikwa visiwani Pemba na Unguja ambapo sio tu uchaguzi mkuu uliendeshwa na kuhitimishwa kwa amani bali pia chama cha CUF kiliyakubali matokeo kwa moyo mkunjufu na kutamka hadharani kuwa kiko tayari kuunda Zanzibar mpya katika serikali ya kitaifa ambayo itaundwa na Rais Shein.
Hii inaashiria kwamba visiwani humo mambo ni shwari na kwamba kila upande umeafiki kwa dhati kusahau yaliyopita na kuganga yajayo kwa umoja wa kitaifa.
Swali: Je, hao ndugu zetu waliokimbilia nje ya nchi wataendelea kuhesabika kama wakimbizi wa kisiasa na kukubalika waendelee kuishi huko waliko kimoja?
Naomba kuwasilisha
Mdau Ilham wa Oman
No comments:
Post a Comment