...

...

Friday, May 21, 2010

HAPPY BIRTHDAY: BC IS THREE YEARS OLD TODAY!

Leo ni siku ya furaha. Ni siku ya kufurahi na kutafakari. BC imetimiza miaka mitatu hivi leo tangu ianzishwe! Ni vigumu kuamini kwamba siku na miaka zinakwenda kwa kasi ya namna hii. Waliosema “siku zinaruka” pengine hawakukosea! Ni vigumu kuamini kwamba tayari miaka mitatu ya kutafuta habari,kupanga miadi,kusaka picha,kuandika,kuhariri,kubandika,kubandua,kukesha au kudamka alfajiri kukamata habari moto moto nk imekatika.

Hatuna mengi ya kusema hivi leo zaidi ya kwanza kumshukuru Muumba kwa kutulinda na kutuwezesha kuwepo hai leo hii. Pili ni kukushukuru wewe mtembeleaji na mchangiaji wa BC. Tunatambuwa wazi kwamba mtandaoni zipo blogs nyingi sana na katika lugha mbalimbali ikiwemo hii yetu ya Kiswahili.Nyingine zina mvuto na rasilimali kuishinda BC. Lakini kwa sababu umechagua kila mara kututembelea na kuchangia mawazo na mtizamo wako hapa, hatuna budi kukushukuru sana sana.

Tunaamini kwamba hiyo ni kwa sababu unaipenda BC na unathamini mchango wake katika ulimwengu wa habari na mawasiliano. Asante sana. Shukrani nyingi pia ziwaendee ninyi nyote ambao mara kwa mara mmekuwa aidha vyanzo vya habari zetu,burudani zetu. Pia shukrani kwa wale ambao wamekuwa wakitukosoa pale tunapoteleza. Tungependa kukuhakikishia kwamba tunathamini sana michango hiyo ikiwemo kukosolewa.Bila kukubali kukosolewa na kujirekebisha,pengine tungeshapotea katika ulimwengu wa blog siku nyingi zilizopita.

Pamoja na hilo, BC kama mojawapo ya vyanzo vya habari au kisima cha kusambaza habari, si kitu bila ushirikiano wa vyombo vingine vya habari na mawasiliano. Kwa hali hiyo ni lazima na sharti tuseme shukrani nyingi sana kwa vyombo vyote vya habari nchini Tanzania zikiwemo radio,magazeti na hata luninga.

Juu ya yote shukrani sana kwa bloggers wenzetu.Bila ninyi kazi ingekuwa ngumu maradufu.Asanteni sana. Shukrani za pekee ziwaendee Mzee wa Libeneke, Ankal Muhidin Issa Michuzi, Ahmad Michuzi, Brother Mubelwa Bandio(nashukuru sana kwa mawazo na michango yako),Haki Ngowi, Bob Sankofa, Shamim Zeze, Maggid Mjengwa,Mrocky Mrocky,John Bukuku,Maxence wa Jamii Forums, Geeque wa BongoRadio na EastAfrican Tube,Yahya Charahani ,kampuni nzima ya Global Publishers wakiongozwa na Abdallah Mrisho na wengine wote. Kama hatujakukutaja hapa sio kwamba sithamini mchango.La! Ni kwamba tumependa kuwapa tuliowataja upendeleo maalumu kwa sababu maalumu. Tunakupenda na tunakuthamini. Tafadhali endelea kufanya unachokifanya. Asante sana.

Shukrani nyingi na za kipekee kwa wadhamini wetu.Bila ninyi ni wazi kazi ingekuwa ngumu zaidi. Asanteni sana.

Tunauanza mwaka mwingine. Kama ambavyo umeshuhudia katika kipindi kilichopita, kikubwa ambacho tunajaribu kujitahidi nacho ni kuboresha kazi zetu. Ni kazi kubwa na yenye gharama zake lakini tumedhamiria kuifanya kwa sababu tunathamini na kuamini katika ulimwengu huru wa habari na mawasiliano. Asanteni.

NB:Kwa niaba ya wadau wa kKaobama mtoto tutakutakia kila kheri katika kuleta burudani kwa wasomaji wote waliko. hakika na idumu!!!

No comments:

Post a Comment