BABU SEYA NA PAPII KUTEKETEA JELA;FRANCIS NA MBANGU WAPO HURU

Ndoto za mashabiki wa muziki kuwaona tena Nguza Viking(Babu Seya) na Papii Kocha(Mwana wa Mfalme) wakilipanda tena jukwaa la uraiani kutoa burudani,hususani katika wimbo wao maarufu wa Seya,leo zimefikia ukingoni.Rufaa yao imekataliwa.Hata hivyo,kwa mujibu wa mtandao wa Global Publishers,watoto wawili,Francis na Mbangu, wameachiwa huru!
Jopo la majaji watatu wa Mahakama ya Rufaa, wakiongozwa na Jaji Natalia Kimaro, Salum Massati baada ya kupitia kwa makini rufaa hiyo, iliyosomwa na Naibu Msajili wa Mahakama ya Rufaa, Neema Chusi, wamewaachia huru vijana hao baada ya kuridhika na hoja za upande wa utetezi kuwa hawakuhusika katika tukio hilo lililohusisha familia hiyo mwaka 2003.
Kwa maana hiyo,Babu Seya na mwanae mmoja Papii Kocha,wamerudishwa Ukonga kuendelea kutumikia adhabu ya kifungo cha maisha inayowakabili.
Picha kwa hisani ya Global Publishers
No comments:
Post a Comment