...

...

Wednesday, November 11, 2009

Kwa mara pili,Illuminata


Kwa mara pili,Illuminata James,anapata nafasi ya kuiwakilisha Tanzania katika medani ya kimataifa ya masuala ya urembo.Safari hii anaelekea nchini China kushiriki katika shindano la Miss International 2009 linalotarajiwa kufanyika tarehe 28 mwezi huu.

Illuminata amepata nafasi hiyo baada ya aliyekuwa aiwakilishe Tanzania,Hidaya Maeda,kushindwa kufanya hivyo kutokana na sababu za kiafya.

Kama utakumbuka,Illuminata ndiye aliyeiwakilisha Tanzania katika shindano la Miss Universe lililofanyikia Bahamas.Kwa bahati mbaya,hakufua dafu.Bila shaka atakwenda kutumia uzoefu alioupata katika Miss Universe ili kuleta ushindi kutoka Miss International 2009.Kila la kheri.
.........................................................................................................
Obamamtoto pia inakutakia kila kheri.!

Kwa hisani ya Bongocerebrity.

No comments:

Post a Comment