...

...

Wednesday, November 25, 2009

IJUE HISTORIA YA THANKSGIVING....!!


Alhamisi ya Nov. 26,yaani kesho tunasherehekea sikukuu inaitwa "THANKS GIVING" Ni sikukuu muhimu kweli kwa hawa wenyeji wetu na tumepewa mapumziko ya siku tatu kuanzia Jumatano. Mimi nimevutwa zaidi na historia yake kuliko sherehe zenyewe. (Ingawa nachukia historia, siasa na vitu kama hivyo).

Rafiki yangu mmoja (mwenyeji na mzawa) aliniambia zamani sana nchi ya Marekani ilikuwa inakaliwa na "WAHINDI WEKUNDU" (Red Indians) na hawa ndio wanaostahili kujiita wamarekani kutokana na asili yao. Enzi hizoo za Ujima, hakukuwa na wazungu, wachina, waafrika wala nini. Nchi nzima ilijaa wahindi wekundu. Ikatokea bwana mmoja kasafiri kutoka Ulaya ya Hispania anaitwa sijui Christopher Columbus (kama nakumbuka vizuri, maana historia na mimi ni tofauti). Ndiye mzungu wa kwanza kufika Marekani na inaaminika ndiye aliyeigundua Marekani. (Nachukia wanaposema mtu kagundua nchi fulani wakati kulikuwa na wenyeji pale, ni sawa na ninavyochukia huyo aliyegundua mlima Kilamanjaro wakati kizazi cha Masawe kilikuwa pale.!!!). Alipogundua kuwa kuna nchi huku akatoa taarifa Hispania kwa wakubwa zake na ndipo walipokuja kuitawala Marekani. Kwa mara ya kwanza walishuka katika jahazi lao Tarehe 23 Nov ya huo mwaka ambao siukumbuki.

Wakafanya bonge la sherehe kwa kusafiri salama na kuanza kuwatawala wenyeji, chakula rahisi walichopata ilikuwa wale ndege wakubwa kwa jina la Bata Mzinga (Turkey). Basi kila mwaka wakawa wanafanya sherehe kukumbuka na kumshukuru Mungu kwa kusafiri salama, kutawala Marekani na kupata chakula cha Turkey. Ikawa mazoea na kila analofanya Bwana ni lazima liigwe na Mtwana. Hata wenyeji nao wakaanza kusherehekea na kumshukuru Mungu kwa kufika kwa wa-Hispania, kutawaliwa na kujipoza na nyama ya Turkey. Ikawa utamaduni na hatimae kupitishwa kuwa sikukuu na tunapewa mapumziko ya siku tatu.!!! Siku hizi yaani usiposherehekea Thanks Giving na kupika Turkey wanakushangaa na kukuona wa ajabu. Ni kipindi pekee (pamoja na X-Mass) wamerekani hukutana na familia zao na kukaa nyumba moja kwa siku tatu.!! Watu wa dini wanadai wanamshukuru Mungu kwa chakula alichowapa mwaka mzima. Rafiki yangu mmoja kutoka India yeye ni Budha aliwauliza yaani nyinyi mnamshukuru Mungu kwa chakula mara moja tu kwa mwaka wakati sisi ni lazima tushukuru kila mlo (mara tatu kwa siku) kweli nyinyi ni watu wa ajabu.!

Mi nachoshindwa kushangaa ni pale hii sikukuu ilivyoanza wakati wa ukoloni na hatimae kuwa siku ya kitaifa. Kwangu mimi ni sawa na watu kusherehekea kutawaliwa kwao na Hispania. Bora niache maana naweza kuandika yasiyostahili bure. Tuonane baadae kuendelea na makala zetu..
H.MTU


......................................................................................................................

No comments:

Post a Comment