...

...

Wednesday, August 26, 2009

MBAGALA NA MAAFA YA MABOMU MBONA WAMESAHAULIWA!



CUF – Chama Cha Wananchi kinashangazwa na serikali ya Tanzania kwa kutowajali wananchi wake hasa pale wanapofikwa na majanga au wanapotakiwa kulipwa fidia kwa ajili ya upotevu na uharibifu wa mali zao au kwa ajili ya mafao yao ya uzeeni, hali hii iliyojitokeza Mbagala iliwatokea pia wastaafu wa Jumuiya ya Afrika Mashariki. Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, William Lukuvi, alitangaza rasmi serikali itatumia zaidi ya bilioni 8 kwa ajili ya kuwalipa fidia zaidi ya nyumba 9,000 zilizokumbwa na athari za tukio la Mabomu April 29 mwaka huu, hii inaonyesha kuwa serikali ilifanya tathimini ya nyumba pamoja na mali zao kwa waathirika. Hivyo basi, haileti maana nyumba yenye thamani ya milioni 13 mwaka 1993 leo hii ilipwe fidia ya milioni 4.3 bila kuzingatia kupanda kwa gharama za ujenzi. CUF - Chama cha Wananchi inaitaka Serikali ifanye tathimini ya uhakika na sio ubabaishaji na izingatie madhara yaliyowafika wananchi na iwalipe fidia ya mali zao kila mmoja na sio kuwalipa nusu harasa ya mali zao zilizoharibika au robo ya mali hizo.

HAKI SAWA KWA WOTE!

No comments:

Post a Comment