...

...

Thursday, August 27, 2009

DUNIA NA MASAA!!


Amani iwe nanyi.
Hii dunia imetengenezwa vizuri kweli na tembea uone. Niliwahi kufundishwa katika somo la Jiografia na niliona wananidanganya tu, lakini sasa nayaona kwa macho. Hii ni ile ishu ya International date line, mabadiliko ya masaa na mwendo wa dunia kuzunguka jua. Ule mstari haujanyooka, umepindapinda zaidi ya mwendo wa nyoka. Wakajidai kutuambia eti hiyo ni kutokana na majira, masaa, na mzunguko wa dunia hauko sawa kwa mwaka. Mi nilimezea tu lakini sikusadiki hata kidogo.!! Kwi kwi kwi kwi kwi kwi

Sasa juzi usiku wa tarehe moja kuamkia mbili mwezi wa nne (April) wakatutangazia kuwa turekebishe saa zetu na kuongeza lisaa limoja mbele.! Eti kulingana na majira ya mwaka yanabadilika. Mwaka wa jana tarehe 28 mwezi wa kumi (October) walituambia turekebishe saa zetu kwa kurudisha lisaa limoja nyuma. Nilipouliza wataalam wakaniambia hivi;- Kila mwaka 1st April tunatakiwa kuongeza lisaa limoja mbele na 28th October tunarudisha lisaa limoja nyuma kukidhi mwendo wa mzunguko wa dunia. Na hii ni kwa watu wote waishio magharibi ya dunia. Loh

Baada ya kurekebisha saa zetu, jua linawaka hadi usiku.! Jana jua limezama saa mbili na nusu usiku. Tofauti ya masaa na Bongo kwa sasa ni 9 hadi 10. wakati sisi tunapata chai ya asubuhi kule Bongo watu wanapakua chakula cha usiku. Hii inanithibitishia kuwa "Mungu ni mbora katika uumbaji"
imeandikwa na mdau wetu
H.MTUMBEI (Houston)

1 comment:

  1. nimefurahi jinsi ulionesha kuwa dunia Mungu amefanya vitu vyake. Yapo mambo mengi ukiyaangalia kwa umakini utashangaa tu jinsi alivyokuwa makini katika uumabaji. Big up God.

    ReplyDelete